Hebrews 11:8-10

8 aKwa imani Ibrahimu, alipoitwa aende mahali ambapo Mungu angempa baadaye kuwa urithi, alitii na akaenda, ingawa hakujua anakokwenda. 9 bKwa imani alifanya maskani yake katika nchi ya ahadi kama mgeni katika nchi ya kigeni; aliishi katika mahema, kama Isaka na Yakobo walivyofanya, waliokuwa pia warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. 10 cKwa maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi ya kudumu ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu.

Copyright information for SwhKC